Header Ads

Bobi Wine azungumza kwa mara ya kwanza kuhusu mateso aliyopitia Uganda



Mwanamuziki maarufu nchini Uganda ambaye amekuwa mbunge Bobi Wine ametanabahisha kwenye ukurasa wake wa Facebook kwamba kikundi cha watu kilimtesa alipokuwa kizuizini, na kwamba hawakubakisha sehemu ya mwili wake kwa mateso.
Bobi Wine

Mbunge huyo kutoka kambi ya upinzani ,ambaye jina lake halisi ni Robert Kyagulanyi anakabiliwa na mashtaka kwa kurusha mawe gari la raisi lililokuwa kwenye msafara wa Rais Yoweri Museveni mwezi uliopita, na kukamatwa August 13 na kuachiliwa wiki iliyopita.Kwasasa Robert yuko nchini Marekani kwa matibabu zaidi kufuatia mateso aliyoyapata.
Jeshi nchini Uganda limekana tuhuma dhidi yake na kuita kuwa ni upuuzi, naye raisi wa nchi hiyo Museveni pia wameziita taarifa za vyombo vya habari nchini mwake kuwa ni habari bandia.
Bobi Wine amesema kwamba anataka kuandika juu ya yale yaliyomsibu kwasababu raisi Museveni na maofisa wa serikali yake walikuwa wanasema juu ya kile kilichotokea katika mji wa kaskazini-magharibi mwa Arua kuwa si ya ajabu".
Ameandika hivi;
Walinipiga,walinipiga na kunipiga kwa buti zao, hawakubakisha sehemu katika mwili wangu ambayo haikuguswa kwa kipigo, hawakubakisha. Waliyapiga macho yangu,pua na mdomo wangu pia. Wakapiga viwiko vya mikono yangu na magoti yangu, watu wale hawana utu hata kidogo.

No comments