Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza
Jimbo Kuu la Mwanza (kwa Kilatini "Archidioecesis Mvanzaënsis") ni mojawapo kati ya majimbo 34 ya Kanisa Katoliki nchini Tanzania na kama hayo yote linafuata mapokeo ya Kiroma.
Chini yake kuna kanda ya Kanisa yenye majimbo yafuatayo: Bukoba, Bunda, Geita, Kayanga, Musoma, Rulenge-Ngara na Shinyanga.
Historia
- 1880: Kuanzishwa kwa Apostolic Vicariate ya Nyanza kutokana na Apostolic Vicariate ya Central Africa huko Sudan
- 1883: Jina kubadilishwa na kuwa Victoria-Nyanza
- 10 Aprili 1929: Jina kubadilishwa tena na kuwa Mwanza
- 25 Machi 1953: Kupandishwa cheo kuwa dayosisi
- 18 Novemba 1987: Kufanywa jimbo kuu la Mwanza.
Uongozi
- Maaskofu wakuu
- Yuda Thaddeus Ruwa'ichi O.F.M. Cap. (tangu 10 Novemba 2010)
- Anthony Mayala (tangu 18 Novemba 1987 hadi kifo chake 20 Agosti 2009)
- Maaskofu
- Vicars Apostolic
- Joseph Blomjous, M. Afr. (25 Juni 1950 – 25 Machi 1953)
- Antoon Oomen, M. Afr. (18 Machi 1929 – 1950)
No comments