Header Ads

Jinsi ya kutengeneza mwili bila kuingia Gym



Inakuaje wadau?

Nimeanza mazoezi ya kunyanyua uzito (I hate saying vyuma) mwaka 2013. Katika mazoezi hua tunasema majukumu ndiyo mchawi wa mazoezi, hivyo majukumu ya chuo yalikua yakinifanya nisiingie gym vile ninavyotaka iwe.
Wakati mwingine unajikuta unakosa pesa ya kuingia gym hivyo unajikuta huna option zaidi ya kukaa nyumbani ukiangalia ulivyoviingiza kwa wiki sita vikipukutika.

Lakini kwa muda nimekua nikitumia njia ambayo inanifanya kuubakisha mwili kwa kuujaza na kuukata.
Best of all, hili zoezi unaweza ukafanya popote na ndani ya dakika 45 (kutegemea na unavyotaka kua challenged).

Ili kuyafikia malengo ya hapo inabidi tufanye haya mazoezi kwa kutumia mtindo unaoitwa Tabata Protocol.

Zoezi tutakalolifanya litakua ni push ups (pushapu).

Na kanuni yetu itakua;

Zoezi moja litajumuisha seti nne.
Seti moja itajumuisha reps 20.
Kupumzika kati ya seti na seti ni sekunde 10.
Kupumzika kati ya zoezi moja na jingine ni dakika moja.

No comments