Wikipedia
PASCHAL DOTTO LUCAS
Bobi Wine azungumza kwa mara ya kwanza kuhusu mateso aliyopitia Uganda
Mwanamuziki maarufu nchini Uganda ambaye amekuwa mbunge Bobi Wine ametanabahisha kwenye ukurasa wake wa Facebook kwamba kikundi cha watu ...
Blog Archive
PASCHAL DOTTO LUCAS
Blog Archive
- September 2018 (1)
- August 2018 (8)
- July 2018 (3)
- June 2018 (1)
- May 2018 (14)
- April 2018 (46)
- March 2018 (150)
- February 2018 (104)
- January 2018 (24)
- December 2017 (39)
- November 2017 (102)
- October 2017 (57)
- September 2017 (190)
BREAKING NEWS
About Me
Hello, my name is Jack Sparrow. I'm a 50 year old self-employed Pirate from the Caribbean.
Learn More →
HABARI
HABARI
Breaking News
Know Us
Naitwa Paschal Dotto Lucas nilizaliwa April 16, kijiji cha Buhingo Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza katika familia ya kikatoliki yenye watoto saba (7) ya Baba aliyekuwa Dreva wa gari ndogo za kubeba mizigo na Mkulima Mzee Lucas Dotto Mpiga na mama mkulima Salome Ng’washi Makaala nikiwa mimi ni mtoto wa sita(6).
Nilisoma shule ya msingi Buhingo darasa la kwanza mpaka la saba mwaka 2001-2007 na nikafaulu kujiunga na shule sekondari ya kata ya Buhingo kwa kidato cha kwanza mwaka 2008, lakini kabla ya matokeo ya serikali nilifanya mtihani wa kujiunga na shule za kanisa katoliki za seminari kwa ajili ya masomo ya awali ya sekondari (Pre-Form One) nikiwa na wenzangu tisa(9) na tukabahatika kufaulu na kuchanguliwa wawili mimi na rafiki yangu Ditrick Magulu kwenda kusoma seminari ya Sayusayu Maswa wakati huo ilikuwa Shinyanga na sasa ni Mkoa wa Simiyu.
Sikuweza kwenda kujiunga na shule hiyo ya seminari kutokana na familia yangu kuwa na kipato kidogo cha kifedha hivyo nikajiunga na shule ya sekondari ya Buhingo ambayo ni ya serikali wakati huo shule za kata zilikuwa zimeshaanza mwaka mmoja kabla.Ilikuwa mwaka 2008-2011 nikisaidiwa kulipiwa ada ya Padre wa kanisa katoliki Mpoland Rev.Fr.Andrew Madry wakati huo akiwa Paroko wa Parokia yetu na mimi nikiwa mtumikiaji wa misa kanisani.
Nilimaliza elimu ya sekondari mwaka 2011 na tulikuwa jumla ya wanafunzi 53 tuliohitimu kwa pamoja na matokeo yetu wote yalianzia daraja la nne(Division IV).Lakini kila mmoja wetu kwa juhudi zake alipambana na suala ya kitabu mpaka wengine wakajiunga vyuo vikuu na fani tofauti tofauti na kuajiriwa na wengine kujiajiri pia.
Mwaka 2012 nilichukuliwa na Padre wa kanisa katoliki Rev.Fr.George Nima Nzungu nikaanza kuishi naye na kumsaidia shughuli mbalimbali za kilimo wakati huo alikuwa Paroko wa Parokia ya Kabila Magu Jimbo kuu katoliki la Mwanza.Mwka huo huo wa 2012 mwezi April alinipeleka kusoma kama mwanafunzi binafsi (Private Cadidates) kurist na kusoma shule ya Kiislamu ya Thaqafa iliyoko Mwanza na kumaliza mwaka huohuo wa 2012. Mwaka uliofuata wa 2013 Nilijifunza na kufahamu kuendesha gari wakati huo,gari ambalo tulilitumia kwenda shambani mara nyingi kushinda huko tukiwa na yeye na vijana wengine nane (8) tukishughulika na kilimo cha Mahindi na Mpunga.
Mwaka 2014 niliomba kusoma chuo cha Serikali cha Utumishi wa Umma Tabora (Tanzania Public Service College (T.P.S.C) kwa masomo ya Tehama(IT)(Information Technology)na nikachanguliwa na kumaliza mwaka huohuo wa 2014.
Baada ya kumaliza nilirudi kwa Fr.Nzungu na kuendelea na kilimo tena na shughuli zingine, na wakati huo tulianza kilimo cha umwagiliaji baada ya yeye kutoka likizo yake Marekani.Kilimo cha umwagiliaji tulikifanyia kandokando mwa mto Simiyu mpaka mwezi Mei 2017 na baadae akasafiri kwenda kusoma Marekani.
Mwezi Julai 2017 nikaanza kuishi na Fr.Steve BikolwaMungu akiwa Paroko wa Nyambiti-Kwimba na baada ya muda akaniambia kutafuta chuo wakati huo nikiwa Dreva wake nikimsaidia kumwendesha kwenda safari tofautitofauti, nje na ndani ya mkoa wa Mwanza .
Tarehe 14 August,2018 nilienda kujiunga na kusoma masomo ya Uandishi wa Habari na Utangazaji huko Arusha chuo cha The Arusha East African Training Institute. Kwa kuwa Uandishi wa habari ndiyo niliupenda sana toka moyoni na nilipenda niifanye kazi hiyo ya uandishi wa habari kwa umakini na kuuhabarisha umma kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii na huku nikivutiwa kabisa na Millard Ayo, Salm Kikeke wa BBC na Fredrick Bundala (SKY WALKER) kwa jinsi wanavyouliza maswali wakati wa mahojiano(Interview).
Paschal Dotto Lucas ni Bloger na Mwandishi wa Habari toka jiji la Mwanza
About Me
Hot News
Labels
- AFYA
- BAD NEWS
- BREAKING NEWS
- BURUDANI
- CONTACT US
- ELIMU
- FAHAMU
- FROM MWANZA
- FURSA
- HABARI
- HABARI ZA KIMATAIFA
- HABARI ZA KITAIFA
- HABARI ZA MASTAA
- KILIMO
- KIMATAIFA
- KITAIFA
- KUMUKUMBU
- MAAJABU YA DUNIA
- MAARIFA
- MAGAZETI
- MAGAZETI LEO
- MAGAZETI YA LEO
- MFAHAMU
- MICHEZO
- MICHEZO KIMATAIFA
- MWANZA
- NEWS
- SIASA
- SIMANZI
- TAARIFA
- TAZIA
- UCHAMBUZI
- UTAFITI
- ZANZIBAR
- ZILIZOBAMBA MITANDAONI
My Instagram
Contact Us
Contact Form
Business
Translate
Popular Posts
-
Kisiwa cha Saanane ( Saanane Island National Park ) ni hifadhi ya taifa la Tanzania na ni hifadhi ndogo yenye eneo la kilomita za mrab...
-
NYUMBA za mfanyabiashara Saidi Lugumi zilizotangazwa kupigwa mnada na kampuni ya udalali ya Yono Auction Mart huenda zisiuzwe kwa sababu mf...
-
Ni habari ya kusikitisha sana iliyogusa kila mtanzania mzalendo mwenye uchungu na maisha ya kil mtu.Picha inaonesha gari la Mh.Tundu Lissu...